Blogger Tricks

SONG'S LYRICS

SONG;  HIVI KWA NINI ?

Intro, Mimi mwenzenu uu, ninajiulizaa, humu moyoni mwangu uu, sipati majibu uu, ninachoomba aa, watu wa Mungu mnisaidie,  nipate majibu uu, ili nirizike ee.
Chorus; Hivi kwa nini ii? x6

Mwenzenu najiulizaaa, mwenzenu najiulizaaa.

Chorus; Hivi kwa nini ii? x6.

1. a. Matendo yashetani yavutia kuliko ya Munguu, hivi kwa nini?
    b. Shetani anawafuasi wengi kuliko Mungu, hivi kwa nini?
    c. Watu wanachochea ugomvi kuliko amani, hivi kwa nini?
Chorus; Hivi kwa ninin ii ? x6

2. a. Matendo mema huelezwa baada ya kifo, hivi kwa nini ii?
    b. Matendo mema hufutwa na baya moja, hivi kwa nini ii ?
    c. Michango mingi kwa msiba na si ugonjwaa.
Chorus; Hivi kwa nini ii ?x6

3. a. Sigara ni hatari kwa afya ya binadamu, hivi kwa nini ii?
    b. Lakini watumiaji ni wengi sana, hivi kwa nini ii?
    c. Israel taifa la Mungu laongoza kwa maovuu.
Chorus; Hivi kwa nini ii ? x6

Mwenzenu najiuliza, mwenzenu najiulizaaa.
Hivi kwa nini ii ? x6

Mimi mwenzenuuu, ninajiulizaaa, humu moyoni mwanguuu, sipati majibuuu. Ninachoombaa watu wa Mungu mnisaidie nipate majibuuu ili nilizikeee.

Song lyrics by Mwl. Henry Sanga.



SONG; BAHARI TULIA.

1. Nilianza safari yang asubuhi na mapema nikitafuta mpenzi wangu mpenzi wa roho yangu.
    Nilitembea nilitembea nikafikakando ya bahari nikakuta mpenzi wangu amevuka kwenda ng'ambo.

Chorus: 
Bahari tulia nimwone mpenzi wangu, bahari tulia nimwone nimpenda, bahari tulia nimwone mpenzi wangu bahari tulia tulia nimwonee.x2

2. Safari inaendelea na sasa ni mchana bahari haijatulia na nimechoka hoi tabani, nasema sikati tamaa japo kuna vikwazo vingi lazima nivuke ng'ambo nimwone mpenzi wangu.
Nasonga mbele sirudi nyuma lazima nifike ng'ambo ile niondokane na shida nyingi zinazokumba roho yangu, magonjwa mengi amani hakuna ujane ukiwa vinanisumbua namuhitaji mpenzi wangu Dakitari wa roho yangu.

3. Na sasa ni machweo mpenzi nimesha mwona na huyu ni Yesu kristo mwokoi wa maisha yangu. yeye mfalme wa amani tabibu wa magonjwa yote pia mume wa wajanr suluhisho la mambo yote.
Sitamuacha hatuta achana kaniokoa na thoruba mbaya aniponya magonwa yote yeye ni wangu milele, sitamuacha milele yote mpaka mwisho wa maisha yangu niruke naye juu kwa baba nifurahi naye milele.

Song lyrics by Mwl. Henry Sanga


No comments:

Post a Comment